Kiongozi mkuu wa kanisa la ufufuo na uzima askofu Josephat Gwajima amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu jijini dar es salaam na kusomewa mashitaka mawili yanayomkabili ikiwemo kutoa lugha ya matusi dhidi ya Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo.
Akisomewa mashtaka wawili yanayomkabili na mawakili waandamizi wa serikali kwa upande wa jamuhuri ambao ni Shadrack Kimaro na Tumaini Kweka, mbele hakimu Wilfred Dyansobera, wamesema askofu Josephat Gwajima alitenda kosa la kwanza la kutoa lugha ya matusi akiwa katika viwanja vya Tanganyika Peakers Kawe jijini Dar es salaam dhidi askofu mkuu wa kanisala katoliki Cardinary Pengo. Wakati kosa la pili ikiwa ni kushindwa kuhifadhi silaha pamoja na risasi wakati akiwa katika hospitali ya TMJ jijini Dar es salaam kinyume na sheria za silaha za moto.
Baada ya hakimu Mh. Wilfred Dyansobera kusikiliza pande zote ikiwemo upande wa jamhuri na upande wa mlalamikiwa, katika makosa yote mawili, baada ya wakili wa askofu Gwajima Dr. Peter Kibatala kuiomba mahakama kumuachia mteja wake kwa dhamana, mahakama iliridhia na kumuachia huru askofu Gwajima kwa dhamana ambapo katika kosa la kwanza amejidhamini mwenyewe kwa kutoa shilingi milioni moja na katika kosa la pili ametolewa kwa dhamana ambapo baada ya mahakama kumuachia huru pamoja na baadhi ya wafuasi wake watatu walikamatwa na kufikishwa mahakamani hapo.
Kabla ya hapo askari wa jeshi la polisi walishuhudiwa wakiwa wamezingira geti la askofi Gwajima nyumbani kwake Salasala hali iliyotia hofu kwa wakazi wa maeneo hayo na viongozi wa maeneo hayo, kama alivyopata kukieleza chanzo hiki, mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kilimahewa kata ya Wazo alipojenga askofu Gwajima.
Askari wakiwa nyumbani kwa Gwajima |
Baada ya askari wa jeshi la polisi kuondoka katika nyumba ya skofu Gwajima, umati ya waumini wake ulimiminika nyumbani kwake ambapo baada ya muda mfupi aliondoka kwenda katika kituo kikuu cha polisi CENTRAL ambapo baada ya kuingia ndani na kukaa kama dakika 10 aliondolewa chini ya ulinzi na kufikishwa katika mahakama ya hakimu Kisutu.
Gari lililombeba Gwajima likitoka nyumbani kwakwe kuelekea kituo cha polisi kwa mahojiano. |
Baada ya kuachiwa huru waumini wake waliofika mahakamani hapo walianza kuimba nyimbo ambapo kwa mujibu wa wakili wa askafu Gwajima anatakiwa kupanda kizimbani tena tarehe 4 mwezi May 2015 akiongozana na wafuasi wake alioshtakiwa nao.
Kundi la wafuasi wa Gwajima wakifika nyumbani kwa Gwajima mara baada ya polisi. |
Chanzo: ITV
No comments:
Post a Comment
TUNAOMBA MAONI YAKO JUU YA HII HABARI HAPA CHINI