,,,,

bar

Monday, 27 April 2015

Breaking News: Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI imetangaza ajira mpya za Mafundi Sanifu wa Maabara na walimu wa shule za msingi na Sekondari Mwaka 2014/2015.... Kutazama majina bofya HAPA.


 Hatimaye Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI), imetoa ajira mpya za walimu wa cheti, shahada na stashahada kwa mwaka 2014/2015.

A: Orodha ya Walimu na Mafundi Sanifu Maabara Ajira Mpya 
 
Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI inatangaza ajira ya wahitimu wa mafunzo ya ualimu na mafundi sanifu maabara katika mamlaka ya Serikali za Mitaa kama ifuatavyo:-



i. walimu wa cheti (Daraja IIIA) kwa ajili ya shule za msingi 11,366; 


ii. walimu wa stashahada 4,151 na shahada 12,490 kwa ajili ya shule za sekondari



iii. mafundi sanifu maabara 264 kwa ajili kusimamia maabara na kuandaa masomo ya sayansi kwa vitendo katika shule za sekondari




B: Utaratibu Ajira Mpya kwa Walimu na Mafundi Sanifu Maabara

Kila mwajiriwa mpya anatakiwa kuzingatia yafuatayo:-

 

i. walimu wenye sifa waliohitimu mafunzo kwa mwaka wa masomo 2013/14 wamepangwa pamoja na walimu wa sekondari wa masomo ya sayansi na hisabati waliohitimu miaka ya nyuma na wameomba kuajiriwa;



ii. kuripoti kuanzia tarehe 01 Mei hadi 09 Mei 2015 kwenye Ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri kwa ajili ya kuajiriwa na kupangwa vituo vya kazi;



iii. kuwasilisha vyeti halisi vya taaluma ya kuhitimu mafunzo, elimu ya sekondari, cheti cha kuzaliwa pamoja na nakala zake;



iv. hakutakuwa na mabadiliko ya vituo vya kazi; na

 

v. fedha za kujikimu kwa muda wa siku saba (7) na nauli ya usafiri wa magari (ground travel) zitatolewa kwenye halmashauri husika baada ya kuripoti.

Bonyeza hapa chini kuangalia majina kulingana na 'Category' zao.
1. Majina ya Ajira za walimu wa cheti (shule za msingi)-2015 <<<BOFYA HAPA>>>

2.  Majina ya Ajira za walimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati,   Shahada (Degree) na Stashahada (Diploma)-2015 <<<BOFYA HAPA>>>

3. Majina ya Ajira za Walimu wa Sanaa na Biashara ngazi ya Shahada (Degree) na Stashahada (Diploma)-2015 <<<BOFYA HAPA>>>  




No comments:

Post a Comment

TUNAOMBA MAONI YAKO JUU YA HII HABARI HAPA CHINI

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Labels

Afya (4) Habari (37) Magazeti (11) Michezo (8) Picha zinazungumza. (6) Sheria (1) Siasa (10) Uhusiano (2)