Jamal Malinzi, Raisi wa TFF |
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametuma salamu za pongezi kwa Mwenyekiti wa klabu ya Young Africans, Yusuf Manji kufuatia timu yake kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2014/2015.
Katika
salamu zake za pongezi, Malinzi amesema kutwaa Ubingwa wa VPL ni jambo
muhimu na sasa wanapaswa kuanza maaandalizi kwa ajili ya michuano ya
kimataifa barani Afrika mwakani.
Klabu ya Young Africans imetwaa
Ubingwa wa Ligi Kuu nchini kwa mara ya 25 (ishirini na tano) mara baada
ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya timu ya Polisi Morogoro
katika uwanja wa Taifa huku ikiwa na michezo miwili mikononi kabla ya
ligi kumalizika.
Timu ya Azam, (ikiwa na pointi 45 na michezo
mitatu mkononi) na Simba (ikiwa na pointi 41 na michezo miwili mkononi)
zinagombania nafasi ya pili na ya tatu.
Timu ya Yanga imetwaa ubingwa huo kwa kufikisha jumla point 55 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote katika mechi zao zilizobaki mkononi, ambapo timu zilizo karibu ni Azama, baada ya michezo yote kama akishinda yote itakuwa na jumla ya point 54, wakati Simba ikishinda michezo yote iliyo nayo mkononi, itakuwa na jumla ya point 47.
No comments:
Post a Comment
TUNAOMBA MAONI YAKO JUU YA HII HABARI HAPA CHINI