Umoja wa Mataifa umesema ni nusu
tu ya nchi duniani zimeweza kuwapatia watoto elimu ya msingi. Katika utafiti
huo uliofanywa na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO), nchi zilizosifiwa kufikia lengo la elimu yamsingi ni
pamoja na Rwanda,Tanzania, Siera Leon, Afganstan na Nepali. India imepata
mafanikio makubwa sana kwa mujibu wa ripoti hiyo mpya ya UNESCO kuhusu elimu
duniani.
Mwaka 2000 kulikuwa na watoto milioni
19 ambao hawako shuleni nchini India, lakini idadi hiyo imepungua sana na
kufikia milioni moja tu, hata hivyo nci hiyo bado inakabiliwa na changamoto
kubwa katika mfumo wake wa elimu. Katika shule nyingi za serikali katika mji
mkongwe wa Delhi, watoto wengi wanatoka katika familia masikini ambapo wanapata
kila kitu shuleni kama vile sare za shule, daftari na vitabu, lakini pia
hawalipi ada za shule. Watoto wengi wa India kwa sasa wanakwenda shule, lakini
wale walio wakubwa hawana budi kutimiza shauku yao ya kusoma na pia kusaidia
familia zao mahitaji. Watoto wengi wanakwenda shule asubuhi na kwenda kazini
jioni katika viwanda vidogo vidogo, wanasema ikiwa hawatafanya hivyo, basi
familia zao hazitakuwa na fedha za kununulia chakula. India imepeleka watoto
wengi sana shule, lakini changamoto yao kubwa ni kuwafanya watoto hao wabaki
shule.
No comments:
Post a Comment
TUNAOMBA MAONI YAKO JUU YA HII HABARI HAPA CHINI