Waganga wa kienyeji wanaotoka katika maeneo tofauti nchini Tanzania wamejitolea kumtibu Msanii WemaSepetu aweze kupata mtoto.
Kulingana
na gazeti la The Standard nchini Kenya Waganga hao waliojitolea
walipiga simu kwa mtandao wa Bongo Movies.com baada ya kukiri kwa nyota
huyo wa filamu kwamba hawezi kupata mtoto.
Wameapa kumtibu tatizo
hilo.''Wajua kuna wanawake wanaopata matatizo madogo kama kutoweza
kupata mtoto licha ya kwamba kuna matabibu wanaoweza kutatua matatizo
yao. Tatizo la wema sio la kumtia wasiwasi, linaweza kutibika''walisema.
"Mpatie nambari yangu ya simu na umwambie anipigie", mmoja wa waganga hao alisema.
Na ili kutaka kujua vile Wema alijibu ombi hilo, inadaiwa kuwa alikubali kusaidiwa na watabibu hao lakini kwa masharti.
''Kuna
wengi zaidi mbali na waganga ambao wamejitolea kunisaidia.nina zaidi ya
ujumbe 400 niliyotumiwa katika mtandao wangu wa WhatsApp huku simu
nyingi zikipigwa.Ukweli ni kwamba niko tayari kupokea usaidizi
huo.'',alijibu.
No comments:
Post a Comment
TUNAOMBA MAONI YAKO JUU YA HII HABARI HAPA CHINI