,,,,

bar

Monday, 6 April 2015

Wilaya ya Butiama, mkoani Mara yakabiliwa na baa kali la njaa.

Image result for nimrod mkono
Mh. Nimrod Mkono



Wilaya ya Butiama mkoani Mara inahitaji msaada wa haraka wa chakula ili kuokoa maisha ya wananchi walio hatarini, baada ya kukabiliwa na baa kubwa la njaa. Hayo yamebainishwa katika kijiji cha Mgango wilayani hapo, baada ya mbunge wa Musoma Vijijini Mh. Nimrod Elirehema Mkono kutembelea kijijini hapo.

"Katika hali ya njaa kijijini kwetu ni mbaya sana, watu wanashindia mapapai pamoja na maembe wengine hata wanalala hivyo bila kula. Kwa hiyo tunaomba serikali kufanya hima ili kusaidia wananchi wa Mgango" Alilalamika mwanakijiji wa kijiji hicho cha Mgango.

Hali hiyo imetokea baada ya majira ya mwaka kubadilika badilika, hata kupelekea misimu ya kilimo kuharibika na mazao mengi yanayolimwa kuharibika kabisa kutokana na kukosa mvua, na hata inaponyesha inachelewa hata kukuta mazao yamekwishaharibika. Wananchi wanaishi kwa kunywa uji kama mlo wao wa kila siku. Ndoo moja ya lita 20 (debe) ya mahindi huuzwa kwa bei ya pesa za kitanzania Sh.15,000, hali ambayo siyo ya kawaida na ni aghali kwa maeneo hayo na kwa mwananchi wa kawaida anayeishi chini ya dola moja kwa siku.

Naye mbunge huyo wa Musoma Vijijini Mh. Nimrod Mkono amekiri kuwepo kwa njaa katika eneo hilo, na amesema tayari amewasiliana na ofisi ya Waziri mkuu kwa ajili ya kuona jinsi ya kutoa msaada wa haraka wa chakula kwa ajili ya kukabiliana na njaa hiyo kali.

Akiongea na wananchi hao, mbunge huyo alisema: "Tuna njaa kubwa hapa Mgango, tutapigana kufa na kupona tupate chakula Mgango. Tayari nimemwambia Waziri Mkuu kwa simu, nataka chakula kiende Mgango".

Hivi karibuni mkuu wa Mkoa wa Mara Kapteni mstaafu Asrey Msangi, kwa nyakati tofauti alimweleza Waziri Mkuu Mh. Mizengo Peter Pinda na Makamu wa raisi Dr. Mohamed Gharib Bilali, kuwa mkoa wa Mara unakabiliwa na njaa kali iliyosababishwa na ukame, pamoja na zao la mhogo kukabiliwa na ugonjwa wa 'bato-bato' kali, hivyo kuhitaji haraka tani zaidi ya 10,000 za chakula.

Wasiwasi huo unasababishwa na misimu zaidi ya mitatu kuharibika bila kupata chakula, ambapo mvua za vuli za mwezi wa pili zinategemewa kwa kupanda, ambapo mazao ya muda mfupi yangevunwa kwa kipindi hiki, na mvua za masika zinazonyesha sasa zimechelewa kiasi kwamba hakuna mazao mengine yatakayopandwa.

No comments:

Post a Comment

TUNAOMBA MAONI YAKO JUU YA HII HABARI HAPA CHINI

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Labels

Afya (4) Habari (37) Magazeti (11) Michezo (8) Picha zinazungumza. (6) Sheria (1) Siasa (10) Uhusiano (2)