NA BASHIR YAKUB-
Upangaji kama upangaji
una mambo mengi.
Hii ndio sababu sheria
imegusa eneo hilo
pia. Kila mtu
anajua kuwa upangaji si
lazima uwe wa
nyumba ya kuishi tu bali hata
ule wa maeneo
ya biashara pia. Ipo
misuguano mingi ambayo
hutokea katika miamala
ya upangaji na upangishaji. Ipo misuguano
inayotokana na ukorofi
tu lakini ipo
misuguano inayotokana na
kutojua baadhi ya
mambo ya msingi
na ya kisheria
kuhusu dhana nzima
ya upangaji na upangishaji . Leo nitaeleza
mambo mawili tu kuhusu
upangaji na upangishaji.
1.INARUHUSIWA KUPANGA
NA WEWE UKAMPANGISHA MWINGINE.
Sheria haimkatazi mtu kupanga
sehemu halafu naye akaamua
kumpangisha mwingine. Hili
lipo na si
kinyume cha sheria
kufanya hivi. Na
zaidi hata huyu
aliyepangishwa naye anaweza
kumpangisha mwingine wa
tatu. Yaani ikawa
A amempangisha B na B
amempangisha C na
C amempangisha D na wote
katika eneo hilohilo.
Hii yote inaruhusiwa
na upangaji wa
kila mmoja unalindwa
na sheria na
kila mmoja anapata haki zake
kwa nafasi yake.
Kwa mfano kila mpangishaji ataitwa
mwenye nyumba yaani
A ataitwa mwenye
nyumba na B
na B ataitwa
mwenye nyumba na
C na C
ataitwa mwenye nyumba
na D. Halikadhalika
kila aliyepangishwa ataitwa
mpangaji.
Suala la msingi
sana katika upangaji
wa namna hii
ni kuwa ule
mkataba wa mwenye
nyumba halisi ambaye
ni mmiliki kabisa yule
A uwe unatoa
ruhusa kwa mpangaji aliyempangisha naye kuruhusiwa kupangisha
mwingine na yule
mwingine naye mkataba
wake umruhusu kumpangisha mwingine na
mwingine naye mkataba
wake umruhusu kumpangisha
mwingine iwe hivyohivyo. Ikiwa
mkataba wa mmoja haumruhusu kupangisha zaidi basi
huyo asiyeruhusiwa hawezi
kumpangisha mwingine na
akifanya hivyo itakuwa
kinyume cha sheria. Kisichowezekana ni
kuwa huwezi kuwa mpangaji halafu
ukampangisha mwingine bila kuwa umeruhusiwa
kufanya hivyo na
mwenye nyumba katika
mkataba wenu.
Lakini pia katika
upangaji wa
namna hii unaohusisha A, B,
C na
D kama tulivyoona ni
lazima kila anayempangisha mtu
wake ampangishe muda mfupi zaidi kuliko
ule aliopanga yeye.
Kwa mfano B amepanga miezi
kumi basi atakapompangisha C
inabidi ampangishe miezi tisa
au chini yake.
Haiwezekani ikawa yeye
alipanga miezi kumi
halafu ampangishe mwingine
miezi kumi na
moja au mwaka au zaidi. Pia
masharti ya upangaji
aliyopewa B ndiyo
hayohayo anayopaswa kumpa
C kama mpangaji
wake. Haiwezekani yeye
aliambiwa asitumie chumba
au uwanja fulani
ikiwa kama sehemu
ya mkataba wake
halafu yeye katika
kumpangisha mwingine akamruhusu
kutumia uwanja au
chumba kile.
Masharti lazima yawe
yaleyale isipokuwa yanaweza
kupungua lakini yasiongezeke. Kwa
mfano B anaweza
kuwa amepanga vyumba
viwili na akapangisha
kimoja lakini hawezi
kuwa amepanga viwili
halafu akampangisha mwingine vitatu. Hivi
ndivyo ilivyo kwa
maeneo yote ya
biashara au makazi.
2. MWENYE NYUMBA
HARUHUSIWI KUFANYA MABADILIKO
YOYOTE BILA TAARIFA MAALUM.
Mabadiliko yaweza kuwa
ya kuongeza kodi,
kuondolewa katika eneo
la pango, kupanda kwa
bei ya huduma
kama umeme, maji,
usafi , kutembelea eneo
la pango kwa
ajili ya ukaguzi, kubadili mfumo
wa ulipaji kodi, kufanya
marekebisho ya ujenzi katika
eneo la pango, na
kila kitu ambacho
ni sharti katika mkataba
wa pango ni
lazima kitolewe taarifa( notice) kabla ya
kukifanyia mabadiliko au
kuongeza kipya.
Kwa taarifa
ya kuongezeka kwa
kodi au kuondolewa
katika pango taarifa
inabidi iwe ya
miezi mitatu. Aidha
mambo mengine kama
taarifa ya kufanya ukaguzi
wa eneo na
mambo mengine yaliyo
katika mkataba yafaa
kukubaliana kimkataba ni
muda gani uwekwe
kama muda maalum
wa taarifa. Kwa mfano
mnaweza kuandika kuwa
mwenye nyumba atatoa taarifa
ya mwezi mmoja
kabla ya kuja
kukagua eneo la
pango.
Na taarifa katika masharti
mengine yaliyo katika
mkataba mnaweza kukubaliana
muda wa taarifa uwe
lini na muda unaweza kutofautiana
katika sharti hadi
sharti. La kuzingatia hapa
ni kuwa hakikisha
unakuwa makini katika kuandaa
au kusaini mkataba wa
pango na ni
muhimu kuwa na
mwanasheria ili kukumbusha
na kuainisha mambo
ya msingi ili
kuondoa lawama na kutoelewana
mbeleni. Leo nimezungumzia mambo
mawili tu siku
nyingine tena nitaeleza
mengine kwani yapo
mengi mno ya kisheria kuhusu upangaji
na upangishaji.
No comments:
Post a Comment
TUNAOMBA MAONI YAKO JUU YA HII HABARI HAPA CHINI