Manny Pacquiao alaumu jeraha la bega alilokuwa nalo kwamba ndicho chanzo cha kupoteza mchezo wake hap oleo alfajiri, dhidi ya mpinzani wake Floyd Mayweather lililofanyika katika uwanja wa Metro Goldlwyn Mayer (MGM) Grand, mjini Las Vegas nchini Marekani.
Pacquiao amelaumu kwamba jeraha hilo lilisababisha asitumie
mkono wa kulia.
Mmarekani Mayweather ,(38) alimchakaza mpinzani wake kutoka
Ufilipino katika uwanja wa MGM Grand na kutunukiwa kwa kuwa na maamuzi mapana
ya umoja.
Pacquiao (36), alisema alifikiri alijiandaa vyema kushinda
pambano hilo, ingawa watazamaji wengi walikubaliana (kuridhika) na na uamuzi.
“Majuma matatu kabla ya pambano hili niliumia bega la mkono
wangu wa kulia” alisema Pacquiao. “Lilipona lakini haikuwa kwa asilimia mia
moja”.
Mayaweather alianza kung’ara kuanzia raundi ya pili, na
kumvurumishia Pacquiao makonde mazito kupitia upande wake wa kulia.
Mfilipino huyo alirudi tena katika raundi ya nne na kumchapa
Mmarekani huyo , Mayweather kupitia
mkono wake wa kushoto, na pia katika raundi ya sita, lakini bado ‘hakufua dafu’
mbele ya Mmarekani huyo, kumelekea kuibuka kidedea katika mpambano huo wa aina
yake. Kama inayoonekana hapa chini.
Mayweather | Pacquiao | |
---|---|---|
Punches throws
|
435
|
429
|
Punches landed
|
148
|
81
|
Jabs thrown
|
267
|
193
|
Jabs landed
|
67
|
18
|
Pacquiao alisema alitaka kuchomwa sindano katika bega lake kabla ya pambano hilo lakini Kamati ya inayomsimamia ya Nevada Athletic ikakataa.
Promota wa Pacquiao, Bob Arum, alilalamika kwamba
aliitaarifu kamati hiyo ya Nevada juu ya jeraha hilo siku tano zilizopita kabla
ya mchezo, na kusema haiwezekani kuahirisha mchezo huo, na kudai ni jambo la
kawaida katika historia ya masumbwi.
“Mpambanaji siku zote hupigana kwa kuumia na tulifikiri kazi
iliyokuwa imefanyika katika bega hilo wakati wa mazoezi ingeweza kumsaidia
kuutumia mkono wake huo wa kulia” alisema Arum.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Francisco Aguilar alisema kwanza
alijua jeraha hilo masaa mawili kabla ya mpambano, wakati kambi ya Pacquiao
walipoomba kuachiwa nafasi ya daktari upande wao, ombi lililokataliwa.
Wakati huo Mayweather, alisema alikuwa na majeraha katika
mikono yake yote na viganja.
“kama angeibuka mshindi, ningemuonesha heshima, na kusema
alikuwa ni mtu makini” alisema baada ya kuongeza makanda wa Pacquiao wa WBO
katika mikanda ya WBC na WBA aliyokuwa akiimiliki.
Mayweather, Bingwa wa dunia wa uzito wa tano, pia aliwakosoa
waliokuwa wana wasiwasi juu yake, nakusema kwamba amewafanya ‘wale maneno yao’.
“Kwa miaka mingi kila mmoja amekuwa akisema kwamba nlikuwa
naogopa na na ningepoteza ambano hili”, alisema Mayweather, amabye hajawahi
kupigwa katika mapambano ya kimataifa 48, kwa miaka 19 ya nyuma.
“Nimewafanya wasioamini kuamini. Nilikuwa mtu bora,
mpiganaji makini – umakini zaidi na, uvumilivu zaidi. Alikuwa akitumia paniki
lakini hakufanikiwa kunfikisha ngumi
nyingi na nimekuwa nikimchapa barabara usoni kwake”.
MAONI YA WAKONGWE……
Bingwa wa dunia wa uzito wa sita, Oscar De La Hayo: “Niite ‘shule-ya-zamani’
napenda mashabiki wanaopata thamani ya pesa zao kwa kutazama mpambano
uliosheheni viteendo. Siko katika masumbwi
ya kukimbia kimbia. Nahisi Kama vile naruka ruka kutoka kwenye kiti
kutokana na mpamabano ulivyokuwa na raha.”
Bingwa wa dunia wa zamani wa ngumi za uzito juu, Lennox
Lewis: “Watu wengine hutaka damu na kukatishwa tamaa pale wanapoikosa. Hatuwezi
kuondokana na ukweli kwamba Floyd ni fundi.”
Mayweather, amabye
alisema aliwasilishiwa
cheque ya Dollar za Marekani
Millioni 100 katika chumba chake cha kuvalia nguo baada ya pambano, pia amedhihirisha
kwamba amepanga kwa kupenda kwake kuiachia heshima na kwamba mchezo wake wa
mwisho wa Septemba hautakuwa waa ubingwa.
Alipoulizwa juu ya kama mchezo wake wa mwisho ni dhidi ya
Mbritania Amir Khan, Mayweather lijibu: “Sijalifikiria
hilo. Ninachotaka kukifanya sasa ni kurudi kupumzika nyumabani”
Baba yake Mayweather ambaye pia ni mwalimu wake, Floyd Sr,
aliwakosoa waliokuwa hawaamini kabla na baada ya pambano.
“ Analipa gharama kwa kuwa mwema na kuwa mzuri zaidi. Wakati
kijana huyu alikuwa akirusha ngumi na kuzikwepa, watu wakaiita hiyo kuwa ni
kero.
“Hawajui masumbwi, hilo ndilo tatizo”.
Beyonce na Jay-Z nao walihudhuria kushuhudia mpambano.
No comments:
Post a Comment
TUNAOMBA MAONI YAKO JUU YA HII HABARI HAPA CHINI