,,,,

bar

Wednesday, 13 May 2015

Raia wa Burundi watoa ya moyoni.

Marais Jumuiya ya Afrika Mashariki wanakutana leo jijini Dar Es Salaam kujadili mgogoro wa kisiasa unaendelea nchini Burundi.

Mkutano huo utakuwa chini ya uwenyekiti wa Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete aliyeuitisha baada ya ujumbe wa mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa Jumuiya hiyo kwenda Bujumbura nchini Burundi wiki iliyopita.

Rais Pierre Nkurunziza ambaye analaumiwa kugombea urais kwa muhula wa tatu, anatarajiwa kuhudhuria mkutano huo, kusikiliza hoja za viongozi wenzake.

Lakini Je nao raia wa Burundi wana maoni gani kuhusu mkutano huo wa marais wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unaoanza leo nchini Tanzania?

SIKILIZA MAONI YAO HAPA CHINI.

Bomba.Com

No comments:

Post a Comment

TUNAOMBA MAONI YAKO JUU YA HII HABARI HAPA CHINI

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Labels

Afya (4) Habari (37) Magazeti (11) Michezo (8) Picha zinazungumza. (6) Sheria (1) Siasa (10) Uhusiano (2)