,,,,

bar

Friday, 10 April 2015

Mgomo: Hatimaye mgomo wa madereva nchini wamalizika.

Waziriri wa Kazi na Ajira, Mh. Gaudensia Kabaka

Hatimaye mgomo uliokuwa umeitishwa na kutekelezwa nchi nzima dhidi ya madereva wote katika kile kinachosemekana ni kulalamikia na kupinga tamko lililotolewa na serikali juu ya dereva kutakiwa kusoma upya kila anapohitaji ku-'renew' leseni yake, umekwisha.

Mgomo huo ulioanza mapema asubuhi ya leo, ulihusisha madereva wote wa mabasi yafanyayo safari zake ndani ya viunga vya jiji la Dar es Salaam maarufu kama daladala, pamoja na yale yafanyayo safari zake kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania na nje ya nchi. Lakini pia mgomo huo kama ilivyokuwa kwa Dar es Salaam, jiji la Mwanza nalo lilikumbwa na hatihati hiyo ya mgomo.

Akituliza sintofahamu hiyo iliyowakumba wananchi waliofika alfajiri kama ada, kutaka kusafiri na kukuta hakuna basi linaloruhisiwa kuingia wala kutoka ndani ya kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoa mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi, Waziri wa Kazi na Ajira Mheshimiwa Gaudensia Kabaka amesema kuwa tamko hilo halijatoka serikalini, wala si sera ya serikali na kusema kuwa hilo ni tamko la Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) ambaye alitaka derereva yeyote anayerejesha leseni yake upya iliyoisha muda wake, kutakiwa kusoma upya katika chuo hicho kabla ya kupewa leseni mpya.

Madereva hao pia walilalamikia  usumbufu wa maaskari wa usalama barabarani wanaokumbana nao katika safari zao, serikali imewaagiza maaskari hao kusitisha usumbufu huo na kukubali kuondoa tochi za barabarani zilizokuwa kero kwa madereva.

Aidha, Waziri Kabaka alisema kuwa tamko hilo lililowataka madereva hao kusoma kwa kutumia pesa zao, dareva aliyeajiriwa hatakiwi kuongeza elimu ya udereva kwa kutumia pesa zake, bali ni jukumu la waajiri wao kugharamia mafunzo hayo. Akisisitiza juu ya hilo Kabaka alisema madereva wote wahakikishe wanapata mikataba ya ajira zao ili kutambuliwa. Hata hivyo serikali imeahidi kukutana na madereva hao tarehe 18 ya mwezi huu ili kuzungumzia mbadala wa elimu hiyo.

Kwa matamko hayo ya serikali, madereva hao walisitisha mgomo wao majira ya saa tisa alasiri na kuanza safari zao kuelekea mikoa mbalimbali na nchi jirani.  

No comments:

Post a Comment

TUNAOMBA MAONI YAKO JUU YA HII HABARI HAPA CHINI

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Labels

Afya (4) Habari (37) Magazeti (11) Michezo (8) Picha zinazungumza. (6) Sheria (1) Siasa (10) Uhusiano (2)