Kufuatia kitendo cha baadhi ya mashabiki kuwashambulia mastaa kwenye kurasa zao mitandaoni kushamili, Staa wa Bongo Movies, Irene Uwoya ameibuka na kuweka angalizo hili kwa followers wake.
"Mamboz! Nataka niulize swali hivi kunamtu nilimlazimisha kuni follow au ni kwa mapenz tuuu? sasa kwanini mtu anataka kuchukua jukumu la mzazi wangu kujifanya anajua sana maisha yangu wakati toka nizaliwe hajawahi kuninunulia ata pipiii!!!
"Sasa ni hivi kusemwa mimi siogopi na matus pia siogopi kabisa coz nimeanza kusemwa toka nipo tumboniii!!! Ila naomba sanaaa mwanangu awe pembeni hausiki ata kidogo tena naomba sanaaa fanyeni yote lakin mwanangu chondechondeee!!!
"Wewe unayesema na nyota ya mchanga ni kweli hujakosea kwa sababu mchanga una thamani kubwa sana ndomana ukizikwa lazima uwekewe mchanga!
"Sasa ambaye anaona amekuja huku ili anitukanie mwanangu naomba atoke haraka staki kuwa na watu wengi wanafiki ni bora kuwa na wachache wenye mapenzi ya kweli na ukikosea wanakwambia kuliko kuwa na wengi kazi yao umbea na majunguuu!!!
"SITAKI kama unajijua ni mmoja wao fanya usepeee!!!!!"
Bomba.Com
No comments:
Post a Comment
TUNAOMBA MAONI YAKO JUU YA HII HABARI HAPA CHINI