,,,,

bar

Thursday, 30 April 2015

TAARIFA YA UKAWA KWA UMMA: WAIBUA HOJA ZIFUATAZO: UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2015 LAZIMA, KIKWETE ASIONGEZEWE MUDA, KURA YA MAONI BAADAE.

Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) leo vimetoa msimamo wao juu ya njama za kuahirisha Uchaguzi Mkuu unaotakiwa kufanyika Oktoba mwaka huu. UKAWA imesisitiza kwamba kuahirisha Uchaguzi Mkuu huo ni sawa na kumuongezea Rais Jakaya Kikwete na Chama chake cha Mapinduzi muda wa kuendelea kutawala Tanzania.

UHUSIANO: Fahamu jinsi ya kumgundua mpenzi wako aliyekusaliti muda mfupi uliopita.

 Image result for love relationship imagesKUNA BAADHI YA WATU WANAYATENDEA HAKI MAPENZI; WAPO MAKINI KWA KILA KITU KATIKA UHUSIANO WAONA HIVYO KUWA KAMA WANAISHI KWENYE PARADISO YA PEKEE. PIA, WAPO WENGINE AMBAO WANAYAONA MAPENZI MACHUNGU, WANAYACHUKIA NA KWA HAKIKA WANALAANI KUKUTANA NA WENZI WALIONAO. Kwa nini?

Ubunifu: Tazama nyumba iliyojengwa kwa kutumia makopo ya maji!


Ikulu yatoa tamko kuwepo kwa njama za kutaka kumdhuru Dr. Reginald Mengi zilizodaiwa kuandaliwa na rais Jakaya Kikwete

Ikulu imekana kuwapo njama zozote za kutaka kumuangamiza Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dk. Reginald Mengi, zilizodaiwa kuandaliwa na Rais Jakaya Kikwete, kwa kile kilichodaiwa kuwashughulikia wanaoihujumu serikali yake na kupanga kumshughulikia.

Magazeti: Soma vichwa vya magazeti ya leo Alhamisi Aprili 30, 2015.

Wednesday, 29 April 2015

Malinzi aipongeza Yanga.

Jamal Malinzi, Raisi wa TFF

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametuma salamu za pongezi kwa Mwenyekiti wa klabu ya Young Africans, Yusuf Manji kufuatia timu yake kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2014/2015.

Majina (Nominee) ya wasanii wa Muziki wanaowania tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Award (KTMA) mwaka 2014/2015.

Majina wasanii watakaowania tuzo za KTMA mwaka huu. 
Hizi ndizo 'Category' za mwaka huu na wasanii wanaowania tuzo za Kili Music Award. 

Waganga wajitolea kumtibu Wema Sepetu...

Waganga wa kienyeji wanaotoka katika maeneo tofauti nchini Tanzania wamejitolea kumtibu Msanii WemaSepetu aweze kupata mtoto.

Tuesday, 28 April 2015

Je, wewe hupatwa na maumivu ya mgongo? Soma utafiti huu>>>>

Sokwe

Watu wenye maumivu ya mgongo wana uwezekano mkubwa wa maumbile ya mgongo wao kuwa sawa na ule wa sokwe.

Monday, 27 April 2015

Sunday, 26 April 2015

Magazeti: Soma vichwa vya habari vya magazeti ya leo Jumapili Aprili 26, 2015

 Haya ni magazeti ya leo Jumapili tarehe Aprili 26, 2015 kama yalivyoandikwa. Wasiliana nasi kupitia whatsapp numba 0789 577004, facebook www.facebook..com/amos matiko. tweeter https://twitter.com/AmosbombaBlog.

Friday, 17 April 2015

Dr. Reginald Mengi avunja ukimya juu ya tuhuma dhidi yake za kutaka kuiangusha serikali, na kumshughulikia Raisi Kikwete.


Mwenyekiti mtendaji wa  IPP DR. REGINALD MENGI ameeleza kushtushwa na taarifa zilizochapishwa  kwenye gazeti la TAIFA IMARA  zikimtuhumu kuwa ana nia ya  kutaka  kuiangusha serikali ya Rais Kikwete na kumshughulikia baada ya kumaliza  muda wake wa uongozi, kunyamaziwa na  ikulu na idara ya habari maelezo  kwa wiki tatu bila kutoa ufafanuzi wowote.


Mahakama nchini Tanzania sasa yakunjua makucha, yaipa Halmashauri ya wilaya ya Urambo adhabu kali kwa uzembe wa daktari wake.

Tokeo la picha la court hummer

Katika hukumu nadra kutolewahapa nchini Tanzania, mahakama Kuu Kanda ya Tabora imeiagiza halmashauri ya wilaya ya Urambo, kulipa fidia ya shilingi milioni 25 kwa Mwamini Adam na mumewe Idrisa Jafari kutokana na madhara waliyopata baada ya uzembe uliofanywa na daktari wa hospitali ya wilaya hiyo alipokuwa akimfanyia upasuaji Mwamini.

Askofu Gwajima afikishwa mahakama ya Kisutu na kusomewa mashitaka mawili ikiwemo la kutoa lugha ya matusi.



Kiongozi mkuu wa kanisa la ufufuo na uzima askofu Josephat Gwajima amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu jijini dar es salaam na kusomewa mashitaka mawili yanayomkabili ikiwemo kutoa lugha ya matusi dhidi ya  Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo.

Sababu hizi hapa zinazosababisha wanaume wengi kujitoa uhai.... Soma utafiti ufuatao...


Wanaume wengi wenye umri kati ya miaka arobaini na 50 wamo katika hatari kubwa ya kujiua kuliko wanawake.

Kijana mmoja kutoka Uingereza ,Simon Jack alifanya utafiti huo baada ya baba yake kujiua katika siku yake ya kuzaliwa miaka 25 iliyopita akiwa na umri wa miaka 44.

Waziri Sitta awafukuza vigogo wa kampuni ya reli nchini (TRL)..... Madeni Kipande Wa TPA amefukuzwa kazi rasmi


SERIKALI imewasimamisha kazi karibu viongozi wote wakuu wa Kampuni ya Reli nchini (TRL), kwa kile kilichoelezwa kuwa hujuma ya mabilioni ya shilingi yaliyotumika kununua mabehewa chakavu.

Thursday, 16 April 2015

Waliojiunga Al-Shabab wajisalimishe.

Serikali ya Kenya imeahidi kuwasamehe wakenya ambao wamepokea mafunzo ya kigaidi endapo watajitokeza katika kipindi cha siku 10 zijazo...

Wednesday, 15 April 2015

YAFAHAMU MAMBO MAWILI MUHIMU YA KISHERIA YANAYOHUSU UPANGAJI NA UPANGISHAJI.



Image result for MPANGAJI



NA  BASHIR  YAKUB-



Upangaji  kama  upangaji  una  mambo  mengi.  Hii  ndio  sababu sheria  imegusa  eneo  hilo  pia.  Kila  mtu  anajua  kuwa upangaji  si  lazima  uwe  wa  nyumba  ya  kuishi tu bali  hata  ule  wa  maeneo  ya  biashara  pia.  Ipo  misuguano  mingi  ambayo  hutokea   katika  miamala  ya  upangaji  na upangishaji. Ipo  misuguano  inayotokana  na  ukorofi  tu  lakini  ipo  misuguano  inayotokana  na  kutojua  baadhi  ya  mambo  ya  msingi  na  ya  kisheria  kuhusu  dhana  nzima  ya  upangaji  na upangishaji . Leo  nitaeleza  mambo  mawili  tu   kuhusu  upangaji  na  upangishaji.

Thursday, 9 April 2015

Utafiti: Mume 1 kati ya 10 hupigwa na mkewe Kenya.

Mmoja kati ya wanaume 10 wa Kenya amepigwa na mkewe ama mpenziwe kulingana na utafiti wa kiafya.

Wanaume walio kati ya umri wa miaka 20 hadi 24 ambao ni asilimia 11.7 wamevumilia unyanyasaji huo na wamekuwa wakifuatiwa kwa karibu na wale walio na kati ya umri wa miaka 40 na

Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizofanikiwa kuwapa watoto elimu ya msingi duniani.



Umoja wa Mataifa umesema ni nusu tu ya nchi duniani zimeweza kuwapatia watoto elimu ya msingi. Katika utafiti huo uliofanywa na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), nchi zilizosifiwa kufikia lengo la elimu yamsingi ni pamoja na Rwanda,Tanzania, Siera Leon, Afganstan na Nepali. India imepata mafanikio makubwa sana kwa mujibu wa ripoti hiyo mpya ya UNESCO kuhusu elimu duniani.

Michezo: Taifa stars yajinasibu

Kocha wa Taifa Stars, Mart Nooij

Licha ya kupangwa katika kundi gumu na timu za Nigeria, Misri na Chad katika michuano ya kuwania kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika 2017 nchini Gabon, kocha wa timu ya taifa ya hapa Tanzania, Mdachi Mart Nooij amesema timu yake haiziogopi timu hizo.

Tuesday, 7 April 2015

Michuano ya CHAN makundi yapangwa

Timu ya Uganda, The Cranes

Tanzania itachuana na Uganda wakati Kenya itakipiga na Ethiopia katika michuano ya kufuzu ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) kufuatia ratiba ya michuano hiyo iliyotolewa na Shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika, (CAF),

Mechi hiyo ya awali itachezwa kati ya Juni 19-21 wakati ile ya marudiano itachezwa kati ya July 3-5 mwaka huu.
Fainali za CHAN zitafanyika nchini Rwanda kuanzia January 16 mpaka February 7, 2016.
Michuano hiyo, kwa mujibu wa ratiba ya CAF, itashirikisha timu 42, ambazo zitashindana katika kanda 6 na fainali zake zitachezwa na nchi 16 tu wakiwemo timu mwenyeji.
Uganda kwa sasa ipo nafasi katika nafasi ya 84 ya viwango vya FIFA, wakati Tanzania ipo nafasi ya 100.
Ratiba ya kufuzu ya CHAN ni kama ifuatavyo:

Kanda ya Magharibi A.
Guinea Bissau vs Mali
Mauritania vs Sierra Leone
Guinea vs Liberia
Senegal vs Gambia

Kanda ya Magharibi B
Ghana vs Ivory Coast
Nigeria vs Burkina Faso
Niger vs Togo

Kanda ya kati
DR Congo vs Jamhri ya Kati (CAR)
Cameroon vs Congo
Chad vs Gabon

Kanda ya Kati Mashariki
Hatua ya awali
Tanzania vs Uganda
Djibouti vs Burundi
Ethiopia vs Kenya

Kanda ya Kusini
Zimbabwe vs Visiwa vya Comoro
Lesotho vs Botswana
Namibia vs Zambia
Msumbiji vs Seychelles
Afrika ya Kusini vs Mauritius
Swaziland vs Angola

Kanda ya Kaskazini
M1 Libya vs Tunisia
M2 Morocco vs Libya

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Labels

Afya (4) Habari (37) Magazeti (11) Michezo (8) Picha zinazungumza. (6) Sheria (1) Siasa (10) Uhusiano (2)